
Mo Music, anayetamba na wimbo wa ‘Basi Nenda’ na ‘Ntazoea’, alisema ameshafanya mawasiliano na msanii huyo na mipango ikienda kama walivyopanga watakamilisha wimbo huo ndani ya mwaka huu.
“Nimemchagua KCEE kwa sababu nakubali kazi zake, lakini pia atanisaidia kibiashara na kunitangaza kimataifa,” alisema Mo Music.
Msanii huyo asiye na ndoto ya kutoa albamu katika maisha yake ya muziki aliwataka wasanii wenzake kuachana na masuala ya ushabiki wa timu, badala yake waungane ili wawe na nguvu moja ya kutangaza muziki wao ndani na nje ya nchi.