Diamond aungana na mastaa nyota wa Afrika kwenye mradi mpya wa One Campaign

CHAMEBOY MEDIA
By -
0

Diamond Platnumz wiki hii alikuwa jijini Lagos, Nigeria kuungana na mastaa wengi wa Afrika kwenye mradi mpya wa taasisi ya One Campaign.

Tofauti na miradi mingine iliyopita, awamu hii mastaa hao walikutana na mwanzishili wa kampeni hiyo muimbaji wa kundi la U2, Bono.
Kupitia mradi huo mpya, Diamond ameungana na mastaa wengine wakiwemo D’Banj, Omotola, Banky W, Victoria Kimani na wengine.

Kwa pamoja walirekodi remix wimbo ‘Strong Girls’ unaohamasisha umuhimu na mchango wa mwanamke kwenye jamii ya Afrika.

“Strong men are always empowering women…… where are my strong women at,” ameandika msanii huyo kwenye picha inayomuonesha akiwa na mastaa hao mbele ya waandishi wa habari.
Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!